AZIMIO LA ARUSHA NA SIASA YA TANU JUU YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA
Imetolewa na Idara ya Habari, TANU, Dar es Salaam, 1967
0
SEHEMU YA KWANZA Imani ya Tanu SIASA YA TANU NI KUJENGA NCHI YA UJAMAA, MISINGI YA UJAMAA IMETAJWA KATIKA KATIBA YA TANU, NAYO NI HII Kwa kuwa TANU inaamini:(a) (b) (c) Kwamba binadamu wote ni sawa; Kwamba kila mtu anastahili heshima; Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, ya Mikoa hadi Serikali Kuu; (d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo yake, ya kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka na wa kukutana na watu mradi havunji Sheria; (e) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake na ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa Sheria;
1
(f)
Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki kutokana na kazi yake
(g)
Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana kwa vizazi vyao;
(h)
Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia muhimu za kuukuza uchumi; na
(i)
Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe, kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa. MADHUMUNI YA TANU
Kwa hiyo basi, makusudi na madhumuni ya TANU yatakuwa kama hivi yafuatavyo:(a) Kuudumisha uhuru wa nchi yetu na raia wake;
2
(b)
Kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara kanuni za Tangazo la Ulimwengu la Haki za Binadamu.
(c)
Kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa na Serikali ya watu ya kidemokrasia na ya kisoshalist;
(d)
Kushirikiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika vinavyopigania uhuru wa bara lote la Afrika;
(e)
Kuona kwamba Serikali inatumia mali yote ya nchi yetu kwa kuondoshea umaskini; ujinga na maradhi;
(f)
Kuona kwamba Serikali inasaidia kwa vitendo kuunda na kudumisha vyama vya ushirika;
(g)
Kuona kwamba kila iwezekanapo Serikali inashiriki hasa katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu;
(h)
Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote, wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali;
(i)
Kuona kwamba Serikali inaondoa kila namna ya dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu;
3
(j)
Kuona kwamba Serikali ya nchi yetu inasimamia barabara njia kuu za kuzalisha mali na inafuata siasa ambayo itarahisisha njia ya kumiliki kwa jumla mali za nchi yetu;
(k)
Kuona kwamba Serikali inashirikiana na dola nyingine katika Afrika katika kuleta Umoja wa Afrika.
(l)
Kuona kwamba Serikali inajitahidi kuleta amani na salama ulimwenguni kwa njia ya Chama cha Umoja wa Mataifa.
4
SEHEMU YA PILI SIASA YA UJAMAA (a) Hakuna Unyonyaji: Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi: haina ubepari wala ukabaila. Haina tabaka mbii za watu: tabaka ya chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali hayapitani mno. Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao, kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe. Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanya kazi, lakini sin chi ya Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza ikapanuka na kuenea.
5
(b)
Njia kuu za uchumi ni chini ya wakulima na wafanya kazi: Namna ya pekee ya kujenga na kudumisha ujamaa ni
kuthibitisha kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu zinatawaliwa na kumilikiwa na Wakulima na Wafanyakazi wenyewe kwa kutumia vyombo vya Serikali yao na Vyama Pia ni lazima kuthibitisha kuwa Chama vyao vya Ushirika.
kinachotawala ni Chama cha wakulima na wafanyakazi. Njia kuu za Uchumi ni: kama vile ardhi, misitu, madini, maji, mafuta na nguvu za umeme; njia za habari, njia za usafirishaji; mabenki, na bima; biashara na nchi za kigeni na biashara za jumla; viwanda vya chuma, mashini, silaha, magari, simenti, mboleo; nguo, na kiwanda cho chote kikubwa ambacho kinategemewa na sehemu kubwa ya watu katika kupata riziki zao au kinachotegemewa na viwanda vingine; mashamba makubwa na hasa yale yanayotoa mazao ya lazima katika viwanda vikubwa. Baadhi ya njia hizi na nyingine zisizotajwa hapa hivi sasa zinamilikiwa au kutawaliwa na Serikali ya Wananchi.
6
(c)
Kuna Demokrasi: Nchi haiwi ni ya Ujamaa kwa sababu tu njia zake kuu au
zote za uchumi hutawaliwa na humilikiwa na Serikali. Sharti Serikali iwe inachaguliwa na kuongozwa na Wakulima na Wafanya kazi wenyewe. Serikali ya Makaburu wa Rhodesia au Afrika ya Kusini ikitawala au kumiliki njia zote za uchumi, hiyo itakuwa ni njia ya kukomaza Udhalimu siyo njia ya kuleta Ujamaa. kweli. (d) Ujamaa na Imani: Lakini Ujamaa hauwezi kujijenga wenyewe. Kwani Hakuna Ujamaa wa kweli pasipo na Demokrasi ya
Ujamaa ni imani. Hauna budi kujengwa na watu wanaoamini na kufuata kanuni zake. Mwana-TANU wa kweli ni Mjamaa, na Wajamaa wenzie, yaani waamini wenzie katika imani hii ya kisiasa na uchumi ni wote wale wanaopigania haki za wakulima na wafanyakazi katika Afrika na po pote duniani. Wajibu wa kwanza wa mwana-TANU na hasa kiongozi wa TANU, ni kutii kanuni hizi za ujamaa hasa katika maisha yake mwenyewe. Na hasa mwana-TANU kiongozi hataishi kwa jasho la mtu mwingine au kufanya jambo lo lote ambalo ni la kibepari au kikabaila.
7
Utimizaji wa shabaha hizo na nyinginezo zinazofuatana na siasa ya ujamaa unategemea sana viongozi kwa sababu ujamaa ni imani na ni vigumu kwa viongozi kujenga siasa ya ujamaa ikiwa hawaikubali imani hiyo.
8
SEHEMU YA TATU SIASA YA KUJITEGEMEA Tunapigana vita: TANU ina vita vya kulitoa Taifa letu katika hali ya unyonge na kulitia katika hali ya nguvu; vita vya kuwafanya wananchi wa Tanzania (na wananchi wa Afrika) watoke katika hali ya dhik i na kuwa katika hali ya neema. Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe, na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena. Mnyonge hapigani kwa Fedha: Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua silaha; kwani silaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na vitendo vyetu ni kama tumekata shauri kwamba bila fedha mapinduzi yetu hayawezekani. Ni kama tumesema, “Fedha ndiyo msingi wa maendeleo. Bila fedha hakuna maendeleo”!
9
Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao ni kwenye fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi, Viongozi wa mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha.
wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA, Bunge, UWT., Vyama vya Ushirika, TAPA na makundi mengine ya wananchi, mawazo yao na maombi yao na matumaini yao ni FEDHA. Ni kama wote tumekubaliana na tunasema kwa sauti moja, “Tukipata fedha tutaendelea, bila fedha hatutaendea”! Mpango wetu wa maendeleo ya miaka mitano shabaha zake kwa kifupi ni shibe zaidi, elimu zaidi na afya zaidi. Na silaha yetu tuliyotilia mkazo sana ni fedha. Ni kama tumesema, “Katika miaka mitano ifuatayo tunakusudia kujiongezea shibe, elimu na afya, na ili kutimiza shabaha hizo tunatumia $ 250,000,000”. Kama tumetaja na tunapotaja vyombo vingine vya kututimizia shabaha hizo tunavitaja kama nyongeza tu; lakini chombo kikubwa katika akili zetu, silaha kubwa katika mawazo yetu, ni FEDHA. Mheshimiwa Mbunge anaposema kuwa wananchi wa sehemu yake wana shida ya maji, je Serikali ina mpango gani wa kuondoa shida hiyo? Jibu analotaka ni kwamba: Serikali inao mpango wa kuwapa maji wananchi wa sehemu hiyo – KWA FEDHA. Mbunge mwingine anaposema kuwa sehemu yake haina barabara au shule au hospitali au vyote, je, Serikali ina mpango gani?
10
Naye pia jibu ambalo angependa kupewa ni kuwa Serikali inao mpango safi kabisa wa kutengeneza barabara au kujenga shule au hospitali au vyote kwa wananchi wa sehemu ya Mbunge Mheshimiwa huyo - kwa FEDHA. Kiongozi wa NUTA anapoikumbusha Serikali kuwa mishahara ya chini kwa wafanyakazi wengi bado ni midogo mno na nyumba wanazolala si nzuri, je, Serikali inao mpango gani? mishahara na kujenga majumba bora - KWA FEDHA. Kiongozi wa TAPA anaposema kuwa wanazo shule nyingi sana ambazo hazipati msaada wa Serikali. Je Serikali ina mpango gani wa kuzisaidia shule hizo, jibu analopenda kusikia ni kuwa Serikali iko tayari kabisa kesho asubuhi kuzipa shule hizo msaada unaotakiwa wa FEDHA! Kiongozi wa Chama cha Ushirika akitaja shida yo yote ya mkulima jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali itaondoa shida hizo za mkulima – kwa FEDHA. Mradi kila shida inayolikabili Taifa letu wananchi tunawaza Fedha, Fedha, Fedha! Mwaka hata mwaka kila Wizara na kila Waziri hufanya makadirio yake ya matumizi – yaani fedha wanazohitaji mwaka huo kwa kazi za kawaida na mipango ya maendeleo. Waziri mmoja tu na Jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali inao mpango maalum wa kuongeza
11
Wizara moja tu hushughulikia pia kufanya makadirio ya mapato. Ni Waziri wa Fedha. maendeleo. Kila Wizara ina mipango mizuri sana ya ya matumizi huwa Wizara zinapoleta makaidirio yao
zinaamini kwamba fedha zipo ila mkorofi ni Waziri wa Fedha na Wizara yake. Na kila mwaka lazima Waziri wa Fedha na Wizara yake awaambie Mawaziri wenzake na Wizara zao kwamba hakuna fedha. Na kila mwaka Wizara zote huinung’unikia Wizara ya Fedha kwa kupunguza Makadirio yao ya matumizi. Kadhalika Wabunge na Viongozi wengine wanapodai Serikali itimize mipango mbali mbali huwa nao wakiamini kwamba fedha zipo ila mkorofi ni Serikali. Lakini kukataa huku kwa Wizara, na Wabunge na Viongozi wengine hakuwezi kuondoa ukweli; nao ni kwamba Serikali haina fedha. Na kusema kuwa Serikali haina fedha maana yake ni nini? Maana yake ni kuwa Wananchi wa Tanzania hawana fedha. Kiasi walichonacho hutozwa kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha shughuli za Serikali hivi sasa na maendeleo mengine ya nchi. Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa fedha tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama Serikali haina fedha zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi. Ukidai Serikali itumie fedha zaidi unataka izipate; na njia ya kuzipata ni kodi. Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi
12
zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi bila kutaka Ng’ombe akamuliwe tena. Lakini kukataa huku kukiri kwamba tunapodai Serikali itumie fedha zaidi nia yetu ni kutaka Serikali iongeze kodi kunaonyesha kuwa tunatambua ugumu wa kuongeza kodi. Tunatambua kuwa ng’ombe hana maziwa zaidi; kwamba hata ng’ombe mwenyewe angependa ayanywe maziwa hayo au yanywewe na ndama wake au yauzwe yamfae yeye na jamaa yake; utashi huo hauwezi kuondoa ukweli kwamba hana maziwa zaidi. Fedha kutoka nje ya Tanzania, Je? Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya kukiri kodi zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo fedha za kutoka nje ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za aina tatu:(a) Zawadi: Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha za bure tu kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa maendeleo. Wakati mwingine shirika lo lote la nje liipe Serikali yetu au Shirika jingine katika nchi yetu msaada fulani kwa ajili ya maendeleo. (b) Mkopo: Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata kutoka nchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni mkopo. Serikali ya nje au Shirika la nje, kama vile Benki, hukopesha
13
Serikali yetu fedha fulani kwa ajili ya kazi zetu za maendeleo. Mkopo huu huwa una masharti yake ya kulipa, kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida. (c) Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa kuliko ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni yanayotaka kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli mbali mbali za uchumi kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni kwamba shughuli yenyewe iwe ni ya faida – kwao – na pia kwamba Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo Tanzania na kuipeleka kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali iwe na siasa wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishi uchumi wao. Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya nchi yetu. Kuna mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili la kupata fedha kutoka nchi za kigeni. Serikali yetu na viongozi wetu wa makundi mbalimbali hawaachi kufikiria njia za kupata fedha kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata ahadi tu ya kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na viongozi wetu hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa neema imekuja au iko njiani inakuja. Tukipata msaada hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; tukipata kiwanda kipya hutangaza; tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au
14
shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda, mara hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha wananchi kwamba, tunaanza mazungumzo ya neema! TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini. Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili. Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo. Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi fedha zao kwa hiari ili zisaidie Serikali kuondoa dhiki. Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo
15
maana japo tungewakamua vipi wnanachi na wakazi wa Tanzania, matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha kutimiza mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna Serikali ambayo yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili kusaidia mataifa yenye dhiki. Serikali ya Dunia nzima. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna Fedha ambazo nchi zenye neema hutoa
huwa kwa wema wao, au hiari yao au kwa manufaa yao wenyewe. Haiwezekani basi, tupate fedha za ktuosha kwa njia hiyo.
MISAADA NA MIKOPO VITAHATARISHA UHURU WETU Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa au mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa nchi yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake yatakuwa nini kwa Uhuru wetu na uzima wetu. Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi, au nyenzo ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada
16
unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila kujiuliza maswali. Kadhalika mikopo. Kweli mkopo ni bora kuliko misaada ya
“bure”. Mkopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya jitihada itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa ni kuonyesha jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba sharti uonyeshe kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta manufaa ya kukuwezesha kuulipa. Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa. Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama tulivyokwisha sema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo wanatakiwa walipe haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu wachache tu. Na Viwanda vya wenye raslimali zao je? Ni kweli tunavitaka. Hata tumepitisha katika Bunge sheria ya kulinda raslimali ya wageni wanaoanzisha mipango mbali mbali ya uchumi katika nchi yetu. Nia yetu na matumaini yetu ni kuwafanya waone kuwa Tanzania ni nchi inayofaa kuingiza raslimali zao. Kwani raslimali yao itakuwa salama italeta faida. Na faida hiyo wenyewe wataweza kuiondoa bila vipangimizi. Tunayo matumaini ya kupata fedha za maendeleo mbali mbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata za kutosha. Lakini hata
17
kama tungeweza kuwaridhika kabisa Wageni hao na Makampuni hayo mpaka yakubali kuanzisha mipango yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi yetu, hivyo ndivyo tunavyotaka kweli? Kama tungeweza kushawishi wenye raslimai wa kutosha kutoka Amerika, na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata faida na kuipeleka katika nchi zao? Hata kama wasingedai Hivi kweli kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali faida yote watakayopata wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo zaidi. tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa letu? Huu Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo shabaha yetu tungeujengaje? Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa misaada na mikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila kuhatarisha uhuru wetu? Waingereza wana methali isimayo “Amlipaye mwimbaji ndiye huchagua wimbo”. Tutawezaje kutegemea nchi za kigeni na Makampuni ya kigeni kwa sehemu kubwa ya maendeleo yetu bila kuzipa nchi hizo na makampuni hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu wa kutenda tupendavyo. Ukweli wenyewe ni kwamba hatuwezi. Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu
ambacho hatuna, kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu ya
18
maendeleo. Tunafanya makosa kudhani kuwa tutapata fedha kutoka nchi za kigeni. Kwanza, kwa sababu kwa kweli hatuwezi kupata Na pili, hata kama fedha za kutosha kwa maendeleo yetu. siasa nyingine za nchi yetu. TUMEKAZANIA MNO VIWANDA Kwa sababu ya kutilia mkazo fedha tumefanya kosa kubwa la pili. Tumekazania mno viwanda. Kama vile tulivyosema “Bila Fedha hakuna maendeleo,” tutakapokuwa na ni kama twasema pia “Viwanda ndiyo Hii ni kweli siku kusema kwamba fedha nyingi, tutaweza maendeleo. Bila viwanda hakuna maendeleo”.
tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha uhuru wetu na
tumeendelea. Tutaweza kusema, “tulipoanza mipango yetu tulikuwa hatuna fedha za kutosha na upungufu huu wa fedha ulitupunguzia nguvu za kuendesha maendeleo yetu haraka zaidi. Lakini leo tumeendelea na tunazo fedha za kutosha”. Tumeendelea,kwa hiyo, tunazo fedha za kutosha”. Yaani fedha zetu zitakuwa zimeletwa na maendeleo. Kadhalika siku tutakapokuwa na viwanda tuna haki ya kusema kuwa tumeendelea. Maendeleo yatakuwa yametuwezesha kupata viwanda. Kosa tunalofanya ni kudhani kwamba maendeleo yetu yataanza kwa viwanda. Ni kosa maana hatuna uwezo wa kuanzisha viwanda vingi vya kisasa katika nchi yetu. Hatuna fedha
19
zinazohitajiwa na hatuna ufundi unaohitajiwa. Haitoshi kusema kuwa tutakopa fedha na kuazima mafundi kutoka nje kuja kuanzisha viwanda hivyo. Kosa hili jibu lake ni lile lile kwamba hatuwezi kupata fedha za kutosha na kuazima mafundi wa kutosha kutuanzishia viwanda hivyo tunavyotaka. Na pia kwamba hata kama tungeweza kupata msaada huo kuutegemea huko kunaweza kukapotosha siasa yetu ya Ujamaa. Siasa ya kualika msululu wa mabepari kuja kuhozi viwanda katika nchi yetu ingefanikiwa kutupatia viwanda vyote tunavyotaka, basi ingefanikiwa pia kuzuia maendeleo ya Ujamaa. Ila labda tuwe tunaamini kwamba bila kujenga ubepari kwanza hatuwezi kujenga Ujamaa. TUMJALI ZAIDI MKULIMA VIJIJINI Vile vile mkazo wa fedha na wa viwanda unatufanya tukazanie zaidi maendeleo ya mijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata fedha za kutosha kuleta maendeleo katika kila kijiji na ambayo yatamfaa kila mwananchi. Tunajua pia kuwa hatuwezi kujenga kiwanda katika kila kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo ya fedha na viwanda katika kila kijiji; jambo ambalo tunajua kuwa haliwezekani. Kwa ajili hiyo, basi, fedha zetu huzitumia zaidi katika miji na viwanda vyetu pia hujengwa katika miji. Na zaidi ya fedha hizi huwa ni mikopo. Japo zijenge shule,
hospitali, majumba au viwanda ni fedha za mikopo. Hatimaye lazima
20
zilipwe.
Lakini ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa kwa fedha
zinazotokana na maendeleo ya mijini au maendeleo ya viwanda. Hazina budi zilipwe kwa fedha tunazopata kutokana na vitu tunavyouza katika nchi za nje. Kutokana na viwanda vyetu hatuuzi na kwa muda mrefu sana hatutauza vitu vingi katika nchi za nje. Viwanda vyetu zaidi ni vya kutusaidia kupata vitu hapa hapa ambavyo mpaka sasa tunaviagiza kutoka nchi za nje. Itapita miaka mingi kabla ya kuweza kuuza katika nchi za nje vitu vinavyotokana na viwanda vyetu. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba fedha tutakazotumia kulipa madeni haya ya mikopo ya fedha kwa maendeleo na viwanda mijini hazitatoka mijini na wala hazitatokana na viwanda. Zitatoka wapi, basi? Zitatoka vijijini na zitatokana na KILIMO. Maana ya ukweli huu ni nini? Ni kwamba wale wanaofaidi maendeleo yanayotokana na Fedha zitatumika fedha tunazokopa sio kwa kweli watakaozilipa.
zaidi katika miji lakini walipaji watakuwa zaidi ni wakulima. Jambo hili linafaa kukumbukwa sana, maana kuna njia nyingi za kunyonyana. Tusisahau hata kidogo kwamba wakaaji wa mijini wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho la wakulima wa vijijini. Hospitali zetu kubwa zote ziko katika miji. Zinafaidia sehemu ndogo sana ya wananchi wa Tanzania. Lakini kama tumezijenga kwa fedha za mkopo walipaji wa mkopo huo ni wakulima, yaani wale ambao hawafaidiwi sana na hospitali hizo. Mabarabara ya lami yako katika
21
miji, kwa faida ya wakaaji wa mijini na hasa wenye magari. Kama mabarabaraba hayo tumeyajenga kwa fedha za mikopo walipaji ni wakulima; na fedha zilizonunua magari yenyewe zilitokana na mazao ya wakulima. Taa za umeme, maji ya mabomba, mahoteli na Karibu maendeleo mengine yote ya kisasa yako zaidi katika miji.
yote yametokana na fedha za mikopo na karibu yote hayana faida kubwa kwa mkulima, lakini yatalipwa kwa fedha zitakazotokana na jasho la mkulima. Tusisahau jambo hili. Japo tunapotaja unyonyaji hufikiria mabepari, tusisahau kuwa bahari ina samaki wengi. Nao hutafunana. Mkubwa hutafuna mdogo na mdogo naye humtafuna mdogo zaidi. Katika nchi yetu twaweza kugawa wananchi kwa njia mbili. Mabepari na Makabaila upande Pia mmoja; na wafanya kazi na wakulima upande mwingine. vijijini upande mwingine.
twaweza tukagawa wakaaji wa mijini upande mmoja na wakulima wa Tusipoangalia tutakuja kugundua kuwa wakaaji wa mijini nao ni wanyonyaji wa wakulima. WANANCHI NA KILIMO Maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi na fedha. Fedha ni matokeo siyo msingi wa maendeleo. Ili tuendelee twahitaji vitu vine: (i) Watu; (ii) Ardhi; (iii) Siasa safi na (iv) Uongozi bora. Nchi yetu ina zaidi ya watu milioni kumi na eneo la eka 362,000.
22
MAENDELEO YATALETWA NA KILIMO Sehemu kubwa ya eneo hili ni yenye rutuba na mvua ya kutosha. Nchi yetu inaweza kutoa mazao ya aina mbali mbali ambayo tunayahitaji kwa chakula na kwa fedha. Mazao ya chakula (na fedha kama tukiyatoa kwa wingi) ni kama vile mahindi, mchele, ngano, maharage, karanga n.k. Mazao ya fedha ni kama vile mkonge, pamba, kahawa, tumbaku, pareto, chai n.k. Pia nchi yetu ni nzuri sana kwa ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku n.k. Pia twaweza kuvua samaki katika maziwa, bahari na mito. Wakulima wetu wako katika sehemu ambazo zaweza kutoa mazao haya, kama si yote walau mawili matatu au hata zaidi. Kila mkulima wetu aweza akaongeza mazao haya ili ajipatie chakula kingi zaidi au fedha nyingi zaidi. Na kwa sababu nia kubwa ya maendeleo ni kupata chakula zaidi na fedha zaidi kwa ajili ya kujipatia mahitaji yetu mengine, ndiyo kusema kuwa jitihada ya kuongeza mazao ni jitihada, na kwa kweli ndiyo jitihada peke yake, ambayo italeta maendeleo, yaani chakula zaidi na fedha zaidi kwa kila mwananchi.
23
MASHARTI YA MAENDELEO (a) Juhudi: Kila mwananchi anataka maendeleo, lakini si kila mwananchi anaelewa na kukubali masharti ya maendeleo. Sharti moja kubwa ni JUHUDI. Twendeni vijijini tuzungumze na wananchi
kuona kama inawezekana au haiwezekani wananchi kuongeza juhudi. Kwa mfano, katika miji, mfanyakazi wa mshahara hufanya kazi kwa saa saba na nusu au nane kutwa kwa muda wa siku sita au sita na nusu kwa juma. Tuseme saa 45 kwa juma, kuondoa majuma Ndiyo kusema mawili au matatu ya livu, katika mwaka mzima. 48 au 50 kwa mwaka.
mfanya kazi wa mjini hufanya kazi ya saa 45 kwa juma kwa majuma
Katika nchi kama yetu muda huu ni mdogo kwa kweli. Nchi nyingi hata zilizoendelea kutuzidi – hufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko saa 45 kwa juma. Si jambo la kawaida nchi changa kuanza na muda mfupi kama huo. Jambo la kawaida ni kuanza na muda mrefu zaidi na kuupunguza kila nchi inavyozidi kuendelea. Sisi kwa kuanza na muda mfupi huu na tunapodai muda mfupi zaidi kwa kweli tunaiga nchi zilizoendelea. Na kuiga huku kunaweza kukaleta majuto. Lakini hata hivyo wafanya kazi wa mishahara hufanya kazi ya saa 45 kwa juma; livu yao kwa mwaka haizidi majuma manne.
24
Yafaa kujiuliza wananchi wakulima hasa wanaume, hufanya kazi kwa saa ngapi kwa juma na miezi mingapi kwa mwaka. Ni wengi mno ambao hawatimizi hata nusu ya wastani wa mfanyakazi wa mshahara. Ukweli wenyewe ni kwamba vijijini kina mama hufanya sana kazi. Pengine hutimiza saa 12 au 14 kutwa. Hawana Jumapili, na hawana livu. Kina mama wa vijijini hufanya kazi zaidi kuliko mtu mwingine ye yote katika Tanzania. Lakini kina baba wa vijijini (na baadhi ya kina mama wa mijini) nusu ya maisha yao ni livu. Nguvu hizi za mamilioni ya kina baba vijijini na maelfu ya kina mama wa mijini ambazo hivi sasa hazifanyi kazi yo yote ila kupiga soga, kucheza ngoma na kunywa pombe, ni hazina kubwa yenye manufaa zaidi kwa maendeeo ya nchi yetu kuliko hazina za mataifa matajiri. Tutafanya jambo la faida kubwa kwa nchi yetu kama tukienda vijijini na kuwaambia wananchi kwamba wanayo hazina hii na kwamba ni wajibu wao kuitumia kwa faida yao wenyewe na faida ya Taifa letu. (b) Maarifa:
Sharti la pili la maendeleo ni MAARIFA. Juhudi bila maarifa haiwezi kutoa matunda bora kama juhudi na maarifa. Kutumia jembe kubwa badala ya jembe dogo, kutumia jembe la kuvutwa na ng’ombe badala
25
ya jembe la mkono, kutumia mbolea badala ya ardhi tupu, kunyunyizia dawa ili kuuwa wadudu, kujua ni zao gani lifaalo kupandwa na zao gain lisilofaa, kuchagua mbegu vizuri kabla ya kuzipanda, kujua wakati mzuri wa kupanda, wakati wa kupalilia n.k., ni maarifa yanayowezesha juhudi kutoa mazao mengi zaidi. Fedha na wakati tunaotumia kuwapa wakulima maarifa haya ni fedha na wakati uletao faida kubwa zaidi kwa nchi yetu kuliko fedha na wakati mwingi tunaotumia katika mambo mengi tunayoyaita maendeleo. Jambo hili kwa kweli tunalifahamu. Katika mpango wetu wa miaka mitano, mipango inayoendelea vizuri na hata kuzidi makisio ni ile inayotegemea juhudi ya wananchi wenyewe. katika muda wa miaka mitatu iliyopita. kwa sababu ya fedha. Kadhalika wananchi kwa juhudi zao wenyewe na maelekezo au msaada kidogo wametimiza mipango mingi sana ya maendeleo huko vijijini. Wamejenga shule, dispensary, majumba ya maendeleo, wamechimba visima, mifereji ya maji, mabwawa, mabarabara, wamejenga mabirika ya kukoshea mifugo na kujiletea wenyewe Pamba, kahawa, korosho, tumbaku, pareto ni mazao yaliyoongezeka kwa haraka sana Lakini ni mazao ambayo yameongezeka kwa sababu ya juhudi na uongozi wa wananchi, siyo
26
maendeleo
ya
aina
mbali
mbali.
Kama
wangengoja
fedha
wasingeyapata maendeleo hayo. JUHUDI NI SHINA LA MAENDELEO Mipango inayotegemea fedha inakwenda vizuri lakini kuna mingi ambayo imesimama na yumkini mingine haitatimizwa kwa sababu ya upungufu wa fedha. Lakini kelele zetu bado ni kelele za fedha. Juhudi yetu ya kutafuta fedha inazidi kuongezeka! Sio kwamba tuipunguze, bali, badala ya safari nyingi ndefu na zenye gharama kubwa za kwenda kutafuta fedha za maendeleo yetu, itafaa kufunga safari kwenda vijijini kuwafahamisha na kuwaongoza wananchi katika kujiletea maendeleo kwa juhudi yao wenyewe. Ndiyo njia ya kweli ya kuleta maendeleo kwa kila mtu. Hii maana yake si kwamba tangu sasa hatutajali fedha, wala hatutajenga viwanda au kufanya mipango yo yote ya maendeleo inayohitaji fedha. Wala siyo kusema kuwa tangu sasa hatutapokea wala kutafuta fedha kutoka nchi za nje kwa ajili ya maendeleo yetu. LA, SIVYO. Tutaendelea kutumia fedha; na mwaka hata mwaka Kwani hiyo itakuwa ni dalili moja ya tutatumia fedha nyingi zaidi kwa maendeleo yetu ya aina mbali mbali kuzidi mwaka uliopita. maendeleo yetu.
27
Lakini hii ni kusema kwamba tangu sasa tutajua nini ni shina na nini ni tunda la maendeleo yetu. Katika vitu viwili hivyo FEDHA na WATU, ni dhahiri kwamba watu na JUHUDI yao ndiyo shina la maendeleo, fedha ni moja ya matunda ya juhudi hiyo. Tangu sasa tutasimama wima na kutembea kwa miguu yetu badala ya kupinduka na kuwa miguu juu vichwa chini. Viwanda vitakuja, na fedha zitakuja, lakini msingi wake ni WANANCHI na JUHUDI yao na hasa katika KILIMO. Hii ndiyo maana ya kujitegemea. Kwa hiyo basi, mkazo wetu na uwe:(a) (b) (c) (d) (a) Ardhi na Kilimo. Wananchi. Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na Uongozi bora. Ardhi:
Kwa kuwa uchumi wa Tanzania unategemea na utaendelea kutegemea kilimo na mifugo, Watanzania wanaweza kuyaendesha maisha yao barabara bila ya kutegemea misaada kutoka nje kwa matumizi bora ya ardhi hiyo. Ardhi ni ufunguo wa maisha ya binadamu kwa hiyo Watanzania wote waitumie ardhi kama ni raslimali yao kwa maendeleo ya baadaye. Kwa kuwa Ardhi ni mali ya Taifa, Serikali ni lazima iangalie kuwa ardhi inatumiwa kwa faida ya
28
Taifa zima na wala isitumiwe kwa faida ya mtu binafsi au kwa watu wachache tu. Ni wajibu wa TANU kuona kuwa nchi yetu inalima chakula cha kutosha na kutoa mazao ambayo yataleta fedha nchini kwa kuuzwa katika nchi za ng’ambo. Ni wajibu wa Serikali na Vyama vya Ushirika kuona kuwa wananchi wanapatiwa vyombo, mafunzo ya uongozi unaohitajika katika kilimo na ufugaji wa kisasa. (b) Watu:
Kuiwezesha siasa ya kujitegemea itekelezwe vizuri, wananchi ni budi wajengwe moyo na shauku ya kujitegemea. malazi. Katika nchi yetu kazi iwe ni kitu cha kujivunia. Bali uvivu, ulevi na uzururaji uwe ni jambo la aibu kwa kila mwananchi. Katika upande wa ulinzi wa Taifa, wananchi wawe macho na vibaraka waliomo nchini ambao wanaweza kutumiwa na maadui wa nje wenye nia mbaya ya kuliangamiza Taifa hili na wawe tayari kulilinda Taifa inapolazimika kufanya hivyo. Wajitegemee katika kuwa na chakula cha kutosha, mavazi ya kufaa na mahali pazuri pa
29
(c)
Siasa Safi:
Msingi wa siasa ya kujitegemea lazima uambatane na siasa ya Ujamaa ya TANU. Ili kuzuia unyonyaji ni lazima kila mtu afanye kazi na aishi kwa jasho lake yeye mwenyewe. Na ili kuleta usawa wa kugawana mapato ya nchi ni lazima kila mtu atimize wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii zake zote. Asiweko mtu wa kwenda kwa ndugu yake na kukaa kwa muda mrefu bila kufanya kazi kwa sababu atakuwa anamnyonya yule ndugu yake. Vile vile mtu ye yote asiruhusiwe kuzurura zurura hovyo mijini au vijijini bila kufanya kazi ya kumwezesha kujitegemea mwenyewe bila kuwanyonya ndugu zake. TANU inaamini kuwa kila anayelipenda Taifa lake ni budi aweze kulitumikia kwa kujitolea nafsi yake na kushirikiana na wananchi wenzake kwa kuijenga nchi kwa manufaa ya watu wote. Ili kudumisha Uhuru wa nchi yetu na raia zake barabara ni budi kujitegemea kwa kila hali bila kwenda kuomba misaada nchi zingine. Kujitegemea kwa mtu mmoja ni kujitegemea kwa nyumba kumi. Kujitegemea kwa nyumba zote kumi za balozi ni kujitegemea kwa tawi zima. Kujitegemea kwa matawi ni kujitegemea kwa Wilaya ambayo ni kujitegemea kwa Mkoa. Kujitegemea kwa Mikoa yote ni kujitegemea kwa Taifa lote ambalo ndilo lengo letu.
30
(d)
Uongozi Bora:
TANU inatambua umuhimu wa kuwa na Uongozi Bora. Tatizo lililopo ni ukosefu wa mipango maalum ya kuwafundisha Viongozi na kwa hiyo Ofisi Kuu ya TANU ni budi itengeneze utaratibu maalum kuhusu mafundisho ya Viongozi tangu wa Taifa zima hadi Mabalozi ili waielewe siasa yetu na mipango ya uchumi. Viongozi ni lazima wawe mfano mzuri kwa wananchi kwa maisha yao na vitendo vyao pia.
31
SEHEMU YA NNE UANACHAMA Tangu Chama kilipoanzishwa, tumethamini sana kuwa na
wanachama wengi iwezekanavyo. Hii ilifaa wakati wa kupigania vita vya kumng’oa mkoloni. Hivyo ndivyo ilivyobidi TANU kufanya kwa wakati huo. Lakini sasa Halmashauri Kuu inaona kuwa wakati umefika wa kutilia mkazo kwenye imani ya Chama chetu na siasa yake ya Ujamaa. Kifungu cha Katiba ya TANU kinachohusu uingizaji wa mtu kwenye Chama kinachohusu uingizaji wa mtu kwenye Chama kifuatwe na ikiwa inaonekana kuwa mtu haelekei kuwa anakubali imani, madhumuni na sheria na amri za Chama, basi asikubaliwe kuingia. Na hasa isisahauliwe kuwa TANU ni Chama cha wakulima na wafanyakazi.
32
SEHEMU YA TANO AZIMIO LA ARUSHA Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka 29/1/67, inaazimia ifuatavyo:A. VIONGOZI 1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au kikabaila. 2. 3. 4. 5. 6. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari. Asiwe na mishahara miwili au zaidi Asiwe na nyumba ya kupangisha. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mawaziri, na Wabunge, TANU, Wakuu wa wa Vyama ya vilivyoshirikishwa Wakuu Mashirika
33
Kiserikali.
Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha (Kwa mujibu wa kifungu hiki
Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu. kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe). B. SERIKALI NA VYOMBO VINGINE 1. Inaipongeza Serikali kwa hatua zote ilizokwisha chukua mpaka hivi sasa katika kutimiza siasa ya Ujamaa. 2. Inaihimiza Serikali, bila kungojea Tume ya Ujamaa, ichukue hatua zaidi za kutimiza siasa yetu ya Ujamaa kama ilivyoelezwa katika Tamko la TANU juu ya Ujamaa. 3. Inahimiza Serikali kutengeneza mipango yake kwa
kutegemea uwezo wa nchi hii kuiendesha mipango hiyo na wala isitegemee mno mikopo na misaada ya nchi za ng’ambo kama ilivyofanya katika mpango wa maendeleo ya miaka mitano. Halmashauri Kuu ya Taifa inaazimia mpango huo urekebishwe ili ulingane na siasa ya kujitegemea. 4. Serikali ione kuwa mapato ya wafanyakazi nje ya Serikali hayapitani mno na yale ya wafanya kazi Serikalini. 5. Serikali itilie mkazo sana njia za kuinua maisha ya wakulima.
34
6.
Inahimiza NUTA, Vyama vya Ushirika, TAPA, UWT, TYL., mashirika yote ya Serikali, kuchukua hatua ili kutekeleza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. C. UANACHAMA
Wanachama wafundishwe kwa ukamilifu imani ya TANU ili waielewe, na wakumbushwe wakati wote umuhimu wa kuishika imani hiyo.